Diamond Analipa Kodi Tsh bil 1.7 kwa Mwaka

Staa wa muziki Tanzania na Africa kwa ujumla Diamond Platnumz ameweka wazi kiasi cha kodi anacholipa kwa mwaka ambapo ni Tsh Bilioni 1.7.

Diamond ameeleza hilo kwenye mkutano wa Zoom ambao umekutanisha wadau wa siasa na viongozi mbali mbali kuelekea miaka 60 ya Uhuru.

“Serikali imetengeneza mazingira rafiki kurasimisha tasnia ya muziki na kuiwekea wepesi kwenda kwenye sekta rasmi, mfano mimi kutoka kwenye uwanamuziki mpaka nimekuwa mkurugenzi wa makampuni mbalimbali”

“Nilikuwa nafanya mahesabu hapa namna ya kimapato huu mwaka kwa kodi ambazo tumezichangia ni Bilioni 1.7, najivunia Serikali imeniwekea mifumo sahihi najiona ni mlipa kodi na nachangia kwa namna moja au nyingine”.


Toa comment