The House of Favourite Newspapers

Diamond ashtuka, agoma kutoa wimbo mpya

ymCTBkpMwanamuziki wa Afro Pop, Diamond Platinum.

MWANAMUZIKI wa Afro Pop, Diamond Platinum anatamani kuachia ngoma nyingine lakini amekiri kupata kikwazo kutokana na matokeo ya Wimbo wa Nana aliouachia mara ya mwisho.

Diamond au Chibu amefunguka kuwa kwenye ‘library’ yake ana nyimbo nyingi kali ambazo zipo tayari kuachiwa muda wowote lakini kutokana na Nana kuendelea kufanya vizuri mpaka sasa tangu alipoiachia anaona bora aendelee kusubiri, asifululize kuingiza kazi nyingi sokoni kwa wakati mmoja.

“Unajua vitu vipya vipo, lakini nimecheki upepo naona kama bado kwanza kwa sasa maana Nana bado inafanya vizuri, nataka kuipa muda kwanza kabla sijaachia ngoma mpya japokuwa nia yangu kubwa ni kuachia wimbo kabla ya mwaka haujabadilika, kwa hiyo bado nacheki,” alisema Diamond.

Nana ambao amemshirikisha Flavour wa Nigeria, umewika vizuri Afrika na kufanikiwa kumpa baadhi ya tuzo ikiwemo ya Wimbo Bora wa Kucheza wa Mwaka (AFRIMMA), Mtumbuizaji Bora (MAMA), Msanii Bora wa Mwaka (MTV EMA), Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (AFRIMA) na nyingine nyingi.

Comments are closed.