The House of Favourite Newspapers

Diamond ‘atajitwalia’ Priyanka Chopra

0

PriyankaMiss Dunia (2000) kutoka India, Priyanka Chopra.
diamond (2)

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

HABARI mjini kwa sasa ni kuhusu tetesi za kuachana kwa ‘flawaz’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Kuna madai kwamba biashara yao imefika tamati baada ya mrembo huyo kutoka Uganda kumzalia Diamond, mtoto aitwaye Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ na kutimkia nchini Afrika Kusini (Sauz).

priyanka chopra (1)Huku bado tetesi hizo hazijakauka masikioni mwa mashabiki, tayari zilishaibuka nyingine kuwa staa huyo anayekimbiza Afrika huenda akamteka Miss Dunia (2000) kutoka India, Priyanka Chopra na kumuweka kwenye himaya yake hasa pale watakapokutana jijini Milan, Italia kwenye Tuzo za MTV Europe Music (EMA).

Katika tuzo hizo, Diamond na Chopra wanachuana katika kipengele kimoja cha Msanii Bora (Best Worldwide Act: Africa/India).

Endapo ni kweli Diamond na Zari ndiyo wamefika Kigoma, mwisho wa reli na amepanga kweli kufanya yake kwa Chopra, swali ni je, atamuweza kulingana na thamani aliyonayo?

priyanka chopra (3)THAMANI YA CHOPRA

Chopra anatajwa kuwa msanii ghali zaidi nchini India akiwa na utajiri unaofikia Dola za Marekani milioni 54 ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni 100 kwa fedha za Kitanzania. Ukiachana na utajiri huo, sifa na jina kubwa alilonalo duniani, mrembo huyo amewahi kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wasanii wenye majina makubwa duniani.

Baadhi yao ni Aseem Merchant (muigizaji) aliyekuwa mpenzi wake wa kwanza ambaye alimwagana naye baada ya msichana huyo kushinda taji hilo la Urembo wa Dunia mwaka 2000. Baada ya hapo, Chopra alinasa kwa mkali wa sinema za Bollywood nchini India, Akshay Kumar kabla ya kuchukuliwa na Harman

Baweja waliyedumu kwa muda wa miaka mitano kwenye uhusiano. Chopra alipomwagana na Baweja alizama kwenye penzi la Shahrukh Khan (mfalme wa filamu India) kisha akahamia kwa Shahid Kapoor ambapo inaelezwa kuwa ameachana naye hivi karibuni hivyo yupo ‘singo’.

diamond (1)DIAMOND UNAANDIKA LAKINI?

Ukweli ni kwamba, kuna kila sababu ya Diamond kujipima ubavu kuwa kipato chake anachoingiza kwenye shoo moja kisichopungua Sh. Milioni 10, umaarufu alionao na mali anazomiliki kutosheleza kumshawishi mrembo huyo aliyewashinda vigogo kama Shahrukh Khan wenye utajiri wa zaidi ya Sh. bilioni 200 za Kibongo.

Ikumbukwe kwamba, kwa wasanii wengi hasa wa kimataifa, uhusiano wa kimapenzi ni moja ya vitu ambavyo vinatakiwa kuwapa chati ili kuwasimamisha kibiashara, sasa ikiwa Diamond, 26, hafurukuti kwa mrembo huyo kwa utajiri, umaarufu na umri, bado swali litabaki palepale kuwa atamuweza?

HISTORIA INAMBEBA DIAMOND

Mbali na vigezo vyote hivyo kuonekana kuwa juu ya uwezo wa Diamond kummiliki Chopra, bado historia inambeba ikimuonesha katika suala zima la mapenzi kuwa ni mtu wa kujaribu na kufanikiwa. Diamond aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mrembo wa Tanzania (2006), Wema Sepetu wakiwa hawaendani hadhi.

Wema alionekana kuwa juu kwani tayari alikuwa ana jina kubwa kitambo, jambo lililochangia  kumpandisha chati Diamond kwa kasi ya ajabu. Huo ni mfano mmojawapo tu unaoonesha kuwa kwa Diamond lolote linaweza kutokea kiasi cha kuonesha maajabu ya kumnasa mrembo huyo mwenye jina kubwa duniani, lakini katika hali halisi Diamond ana kazi kubwa ya kujibu swali kwa kudhihirisha kuwa anamuweza mrembo huyo pale atakapommiliki?

Leave A Reply