The House of Favourite Newspapers

Diamond avuta tuzo 3, Vanessa 1

0

DIAMOND

Diamond Platnumz akiwa na mojawapo ya tuzo alizojishindia jana.

STAA wa Ngoma ya Nana, Diamond Platnumz pamoja na Vanessa Mdee usiku wa kuamkia leo ilikuwa kama sherehe ya ‘x-mass’ kwao baada ya kila mmoja kuvuta Tuzo za All Afrika Music (Afrima) zilizofanyika katika Jiji la Lagos, Nigeria.

sauti sol na diamond

Diamond akiwa katika pozi na Sauti Sol.

Katika tuzo hizo, Diamond aliibuka kidedea kwa kuzoa tuzo tatu moja katika kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka nyingine Wimbo Bora wa Mwaka na Msanii Bora wa Kiume wakati Vanessa akijizolea katika kipengele cha Wimbo Bora wa Pop kupitia Wimbo wa Hawajui.

v money

Vanessa Mdee akipokea tuzo yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliwapongeza mashabiki wake wote waliompigia kura kwa kuandika; “Hii ni kwa ajili yenu mashabiki zangu wote. Asante.”

v money 2

Naye Vanessa kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika; “Utukufu kwa Mungu kwa kuwa juu. Asante sana Nahreal na Barnaba kwa Ngoma hii ya Hawajui.”

Leave A Reply