The House of Favourite Newspapers

Diamond Awatunuku Wizkid, Tiwa Sawage, Wampa Tano – Video

STAA wa muziki Barani Afrika anayetokea nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kwa jina la Wizkid ameeleza kuwa alichokifanya Diamond kupitia Tamasha la Wasafi usiku wa kuamkia jana ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wa Afrika.

 

Wizkid ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 11, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam ukiwahusisha wasanii walioshiriki tamasha hilo.

 

Amesema tamasha hilo ni mfano mwingine wa kuonyesha wasanii wa Afrika ni kitu kimoja na wanashirikiana katika kazi.

“Sijaja kwa sababu nampenda Diamond au naipenda Tanzania, bali nimekuja kwa sababu ni tamasha ambalo limewaunganisha wasanii wa Afrika.”

 

“Hii ni hatua kubwa kwa wasanii kushirikiana na kuungana mkono na inavutia kuona wasanii wanashirikiana. Endeleeni kuunga mkono muziki wa Afrika ili ufike mbali zaidi,” amesema Wizkid.

 

Kwa upande wake, Tiwa Savage ameisifia Tanzania kuwa ni nchi yenye watu wakarimu na upendo mkubwa kwa wasanii wao.

 

Diamond amewapa tuzo wasanii hao wa Nigeria, Wizkid na Tiwa kwa kuungana naye katika Tamasha hilo lililotikisa Afrika Mashariki.

 

Comments are closed.