The House of Favourite Newspapers

DIAMOND, HARMONIZE, RAYVANNY NGOMA NZITO… MONDI ATATESEKA SANA!

DAR ES SALAAM: NGOMA ni nzito! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia madogo kutoka familia ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvann’ kutunisha msuli wa kimafanikio na kumfanya bosi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa katika wakati mgumu.

 

Wadau mbalimbali wa burudani Bongo, wameeleza kuwa, Diamond au Mond kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kutokana na vijana hao kufanikiwa kwenye maeneo mengi ambayo kimsingi kama wataendelea na kasi hii, wanakwenda kuuangusha ufalme wa Diamond uliodumu yapata miaka 10 sasa.

“Diamond amedumu kwenye gemu karibia miaka kumi sasa akiwa juu, lakini kwa sasa mambo yanaonekana kumwendea kombo, anashuka huku vijana wake wakimwashia taa nyekundu,” alisema Wilbefoce Ngoto, mtangazaji wa ITV.

 

UCHUNGUZI WA IJUMAA

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Ijumaa ulibaini kuwa, Harmonize au Harmo na Rayvann au Vanny kwa sasa wanapata shoo nyingi kuliko hata Diamond husususan zile za nje ya nchi na hata za ndani.

Mfano hai, Ijumaa linafahamu kuwa Harmonize ana shoo za mfululizo kuanzia Aprili 16 hadi Novemba 30, mwaka huu. Aprili 16 alikuwa Kenya, Aprili 20 atakuwa Uganda, Aprili 27 (Combani Mayotte) na Mei 3 atakuwa Songea.

 

LISTI NI NDEFU…

Listi bado inaendelea, Juni 6 (Mtwara), Juni 8 (Bahrain), Juni 22 (Sudani ya Kusini), Julai 6 (Tanga), Julai 12 (Canada), Julai 13 (Chicago), Agosti 3 (Ujerumani), Agosti 10 (New York), Agosti 16 (Dalas), Agosti 17 (Califonia), Agosti 24 (London) na Agosti 31 (Seato).

Kama hiyo haitoshi bwa’mdogo huyo atafanya makamuzi mfululizo Oktoba 4, 5 na 6 huko Australia na Novemba 15 atakuwa Dubai na kumalizia mpango mzima Novemba 30 nyumbani Bongo.

UPANDE WA RAYVANN

Kwa upande wa Rayvann, naye anatarajia kupiga shoo kubwa nje ya nchi ikiwemo ya Juni 28, mwaka huu Toronto, Marekani huku Juni 29 akikamua Edmonton, Canada. Kwa upande wake Diamond, anazo shoo kama hizo, lakini ni chache kulinganisha na ile kasi aliyokuwa nayo mwanzoni.

 

MASHABIKI

Mbali na eneo la shoo, Ijumaa limebaini kwamba Harmonize na Rayvann wanammbana vilivyo mbavu Diamond katika kukusanya mashabiki kwani kwa sasa wamekuwa na mvuto wa kujaza kumbi kubwa au uwanja wa mpira, jambo ambalo halikuwahi kutarajiwa kabla.

Hiyo imejidhihirisha pia kwa kitendo cha Diamond kuamua kufanya kolabo zaidi na vijana wake ili kuweza kuwapata mashabiki wao na ndiyo maana nyimbo kama Tetema na Kwangwaru amefanya na vijana hao na zimekuwa zikifanya vizuri sana.

 

KLABU NDIYO BALAA

Vijana hawa wawili kwa sasa wameonekana kuja kwa kasi katika kuvuna mashabiki ndani ya muda mfupi huku wakionekana kumsogelea kaka yao huyo ambaye amewatangulia kimuziki kwani hata nyimbo zinazochezwa klabu mara nyingi si zile za Diamond peke yake bali zile alizoshirikishwa na vijana hao huku zaidi zikipigwa za vijana pakee.

 

INSTAGRAM

Takwimu za kwenye kurasa zao za Instagram zinaonesha Harmonize na Rayvann wanakuja kwa kasi kwani kwa sasa wanajaribu kumtafuta Diamond. Wawili hao kwa sasa kila mmoja ana wafuasi milioni 3.2 huku Diamond akiwa na milioni 6.5.

ULINZI WAO USIPIME

Ijumaa pia limebaini vijana hao walio chini ya Diamond kwa sasa nao wamekuwa wakubwa kiasi cha kuwa na ulinzi kama ambao bosi wao amekuwa nao pindi anapokuwa kwenye shughuli mbalimbali za kimuziki.

Harmonize na Rayvann kwa sasa wanakuwa na baunsa wasiopungua watano au sita ambao wana kiwango kilekile alichokuwa nacho Diamond huku wakiwa na msururu wa wapambe wakiwemo pia mameneja.

 

KUNA LAVALAVA, MBOSSO NA QUEEN

Ijumaa pia limebaini kwenye Lebo ya Wasafi ngoma ni nzito katika kuhakikisha unakuwa juu kwani mbali na Harmonize na Rayvann kuna wasanii wengine wakali ndani ya kruu hilo akiwemo Mbwana Yusuph ‘Mbosso’, Abdul Idd ‘Lavalava’ na Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ ambao nao wanafanya vizuri.

 

Uchunguzi wa Ijumaa umebaini siri kubwa inayowafanya vijana hawa wazidi kutusua na kuweza kumpa presha kaka yao ni uongozi mzuri wa mameneja unaowasimamia kwani unawatengeneza wanapata hadhi ya kufanya vizuri nje nchi zaidi pamoja na ndani.

Uongozi huo unaonekana kuwa na mipango thabiti inayowafanya Wasafi waendelee kuwa juu lakini linapokuja suala la ushindani wa msanii mmojammoja, Diamond anatakiwa kuwa macho na vijana wake kwani kwa sasa wanaonekana kukimkalisha vibaya!

Stori: ERICK EVARIST, IJUMAA

RC MWANRI TENA: KAMATA OFISA HUYU, SUKUMA NDANI!

Comments are closed.