The House of Favourite Newspapers

DIAMOND KAKUBALI KUJISHUSHA, VIPI KIBA?

MARA kadhaa nimekuwa siyo muumini wa kuamini kwamba eti Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wakikubali kukaa chini kwa pamoja na kumaliza tofauti zao basi mmoja wapo atashuka kimuziki, nasema sitaki kuamini kwa sababu ninavyojua kila mmoja kati yao ana ladha yake kwenye gemu la muziki, kila mmoja ana mashabiki na wapenzi wake ‘fact’ yangu ni hiyo.

Hivyo basi ifike hatua tuwaache hawa watu wawili wamalize tofauti zao wenyewe, tuachane na team zisizokuwa na maana ili waendelee kuipeperusha vyema bendera yetu ya Taifa, licha ya kwamba bado inaonekana King Kiba amekuwa mgumu f’lan kujishusha kwa mwenzake lakini Diamond ameonesha wazi kuwa naye kitu kimoja. connections za wasanii wote Afrika ninazo, aje tufanye kazi, nitamsaidia,” alisikika Diamond ambapo kwa upande wa Kiba hakuna jibu lolote lililotoka na baadaye iliachiwa video ya Aje iliyotengenezwa na Dairekta Meji Alabi kutoka Nigeria.

NDOA

Aprili, mwaka huu Diamond alijishusha tena kwa Kiba baada ya kusikia amefunga ndoa na mchumba wake, Amina Khalef huko Mombasa,  Kenya. Kupitia chaneli yake ya Wasafi TV, Diamond alimpongeza msanii huyo kwa kuchukua jiko na kupitia kwenye ukurasawao wa Instagram unaomilikiwa na lebo yake ya Wasafi Classic Baby, uliandika;

“Congratulations Alikiba on your wedding, kutoka Wasafi TV tunakutakia kila la kheri kwenye maisha mapya ya ndoa. Mabrouk!” Lakini napo Kiba hakuonyesha kushukuru kwa lolote zaidi ya kukaa kimya.

LEADERS

Wiki chache mbele, Diamond akajishusha tena kwa Kiba baada ya kutokea kuaga mwili wa aliyekuwa video vixen Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ katika Viwanja vya Leaders jijini Dar. Katika siku hiyo ambayo Kiba alikuwa wa kwanza kufika na kuketi, Diamond aliingia na moja kwa moja akaelekea eneo ambao yupo Kiba na kuanza kuwasalimia wote, alipofika kwa Kiba hakuonesha kupendezwa na salamu yake, akamsalimia kwa kuugeuza mkono jambo lililoleta gumzo.

WASAFI FESTIVAL

Hii imetokea wiki chache zilizopita ambapo Diamond alikuwa akizindua rasmi tamasha lao kubwa litakalokuwa likitoka kila mwaka. Katika uzinduzi huo, Diamond aliongea na waandishi wa habari na kueleza litakavyokuwa na mwisho alimualika Kiba kuwepo naye kwenye tamasha hilo linalotarajiwa kuanza Mtwara, Novemba 24, mwaka huu.

“Hili ni tamasha la kwetu wote, msanii yeyote ambaye atakuwa tayari kushirikiana na sisi lazima tutashirikiana naye, mpaka kaka yangu Ali Kiba ningependa kumuona anashiriki katika Wasafi Festival,” alisema Diamond. Baada ya kupita siku moja, Kiba alimjibu Diamond kisanii kwa kutangaza kinywaji chake cha Mofaya;

“Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani. “Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine.

“Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa. Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa.”

MAKALA: MEMORISE RICHARD

Comments are closed.