Diamond, Kifaa Kipya Gumzo Insta! -Video

MKALI wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amezua gumzo na kifaa kipya ambacho bado hakijajulikana jina lake.

Kupitia ukurasa wake, Diamond ameposti kipande cha video kinachomuonesha akiwa ndani ya gari lake jipya aina ya Escalade akiimba wimbo wake mpya ambao bado hajauachia unaokwenda kwa jina la Loyal.

Diamond ameonekana akimgeuzia kamera mrembo huyo akimuimbia wimbo huo hasa pale aliposema:
“I promise to be loyal…”

Kuna asilimia kubwa huwenda huyu akawa ndiye mpenzi wake mpya kwani watu wake wa karibu akiwemo Juma Lokole amekomenti kumpongeza na kumkaribisha mrembo huyo.

“Karibu shemeji hatutaki ngozi chafu tena pumbavu, mtoto nyororo,” ameandika Juma Lokole.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)


Toa comment