The House of Favourite Newspapers

Diamond Kupandishwa Mahakamani Tena

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

WAKATI sakata la matunzo ya mtoto kwa mzazi mwenza, Hamisa Mobeto likiwa limefifia, jingine limeibuka kwa staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufikishwa mahakamani Juni 20, mwaka huu baada ya mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Gladys Butoto, ambaye ni raia kutoka Kenya kuibuka na kudai kutopata msaada wowote wa malezi ya mtoto anayedai kuzaa na msanii huyo.

 

Akizungumza kwa uchungu nje ya Kituo cha Polisi, Oysterbay, Gladys ambaye ana mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyempa jina la Patiance, alisema kuwa amejitahidi kwa kadiri awezavyo akutane na Diamond ili wayamalize na ijulikane ni jinsi gani wataweza kumhudumia mtoto wao lakini imeshindikana.

 

“Mimi nisingefikia hatua hii kabisa, lakini nimeona Diamond ni mtu ambaye ananidharau na wakati ukweli anaujua, maana tungezungumza na tukakubaliana kuhusu matunzo ya huyu mtoto wala nisingekuwa na matatizo yoyote yale,” alisema Galdys

Msichana huyo ambaye kwa sasa analala nje ya kituo hicho cha polisi alisema kuwa, mara ya kwanza alipokuja nchini alikuwa tayari kupima vinasaba ‘DNA’ yeye, mtoto na Diamond lakini siku ya kupima msanii huyo hakutokea hivyo ilimbidi arudi Kenya.

 

“Nilikaa kidogo Kenya na kuona kwa nini niteseke na mtoto wakati baba yake yupo hai ndiyo maana nimeamua kuja tena kwa mara nyingine, hapa nilipo nimeuza simu yangu na kuja ili nijue hatma ya hili jambo.

“Mwanangu anaumwa lakini nimekuja naye hivyohivyo ili nijue hatma yangu na pia twende mbele ya sheria maana hata mama yake alishawahi kusema mimi ni chizi lakini siwezi kumsingizia mwanaye hata kidogo kuhusu hilo,” alisema mwanamke huyo akionesha barua za kumburuza Diamond mahakamani.

STORI: IMELDA MTEMA, RISASI JUMAMOSI 

MOBETO: NYUMBA TUNAYOISHI IMETOKA KWA DIAMOND – VIDEO

Comments are closed.