Diamond kuwasha moto Dar Live

ymCTBkpDiamond Platinumz.

KWENYE bodaboda, bajaj zote za town, redioni, luningani na kwenye mitandao mingi inazungumziwa pini mpya ya Utanipenda, kitu kipya cha Diamond Platinumz maarufu mitaani kama Baba Tiffah.

Wakati hayo yakiendelea, mwishoni mwa wiki iliyopita, yeye na mpenziwe, Zarinah Hassan au Mama Tiffah, wakafanikiwa kujiongezea tuzo nyingine ya ASFA 2015 katika kipengele cha Best Couple ya Afrika Mashariki, zilizotolewa Uganda.

Ukiachana na hiyo tuzo na nyingine nyingi alizokomba na ngoma kibao zilizohit mwaka huu, Diamond ameamua kurudisha shukurani kwa kuruka na mashabiki wake kabla mwaka haujabadilika.

Mchongo mzima wa kuparty na kuimba na staa huyo utakuwa pale kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala-Zkahem, Dar katika Sikukuu ya Krisimas, Desemba 25, mwaka huu.

Siyo shoo ya kukosa kwa kuwa tayari Diamond ameshaahidi sapraiz kibao lakini kubwa ni lile la kupiga shoo ‘live’ na ku-perform mara mbili zaidi ya alivyowahi kufanya kwenye majukwaa mengine siku za nyuma.

Mitandaoni hakukaliki
Tangu kuachiwa kwa ‘chupa’ ya ngoma hiyo Ijumaa iliyopita, gumzo liliibuka kwenye makutano ya wengi kule mitandaoni kupitia WhatsApp, YouTube, Facebook, Twitter na Instagram zinakopatikana timu za kila aina kila mmoja akizungumza lake kwa namna msanii huyo alivyompagawisha kupitia ngoma hiyo inayotabiri maisha ‘mabovu’ atakayokutana nayo baada ya kufulia hapo baadaye.

Kama hiyo haitoshi, kutua kwa ngoma hiyo ni kama kumeamsha hisia za wengi kutaka kumshuhudia jukwaani Chibu lakini kwa bahati iliyoje, shoo ya karibu ipo Dar Live, cha msingi ni kuvuta subira kwa ajili ya kushuhudia mzigo wa uhakika siku hiyo.

Msikie Diamond
Licha ya kwamba hajawahi kuwaangusha mashabiki wake kwenye shoo tangu apate umaarufu takriban miaka sita iliyopita, lakini safari hii ameahidi kufanya mara mbili zaidi ya anavyofanya akiwa kwenye majukwaa mengine katika siku za nyuma
“Waje tu wengi, sijawahi kuwaza kuwaangusha watu wangu, najua Watanzania wanataka nini na nipo hapa kwa ajili ya kuwafurahisha wao na kuzidi kuipeperusha bendera ya Tanzania. Nitafanya zaidi ya huko nyuma, nataka kufunga mwaka kwa staili ya pekee.

“Hizo sapraiz nilishaahidi tangu mwanzo na siku zinavyozidi kwenda ndiyo mizuka inazidi kupanda, sitaki kuongea mengi, tukutane Desemba 25 pale Dar Live,” alisema Diamond.

Msagasumu huyu hapa
Mkali wa Singeli, Msagasumu anakosa vipi kwenye shoo ya kibabe kama hiyo? Atatia timu na atakamua ngoma zake zote kali zinazotamba mitaani. Nyimbo kama Inaniuma Sana aliyomshirikisha lejendari Juma Nature, Huyo Mtoto, Shemeji Unanitega, Naipenda Simba na nyingine kibao.

“Wanangu wote tukutane pale Dar Live, itakuwa usiku wetu wote. Ngoma zote kali nitatwanga kama kawa, waje wengi turuke pamoja, tufurahi,” alisema Msagasumu.

Wakali Dancers nao wapo
Kundi linalosifika kwa sarakasi na kucheza muziki wa kila aina, Wakali Dancers, nalo litakuwa ndani ya nyumba siku hiyo kukinukisha na kupagawisha uwanja mzima kwa mashabiki watakaojitokeza. Wametamba kuwa itakuwa si ishu ya kitoto kwani wataonyesha mashabiki mbwembwe zao zote zikiwemo zile za kujikunjakunja kwa staili kibao na kudansi ngoma za kisasa za ndani na nje ya nchi.

“Sina mengi ya kueleza kuhusiana na shoo baabkubwa tutakayoifanya Dar Live hiyo Desemba 25, michezo yote ya hatari itafanyika siku hiyo, kutoa burudani ndiyo zetu. Kwa atakayekosa atajilaumu, tutafanya kila kitu kwa ajili ya kufunga mwaka,” walitamba memba wa kundi hilo.

Loading...

Toa comment