Diamond Mabodigadi Hadi Msibani?

MBWEMBWE za staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutembea na mabogadi hadi msibani zimeelezwa ni aina f’lani ya ushamba.

 

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Diamond alizua minong’ono alipohudhuria msiba wa baba wa mmoja wa vijana wake, Don Fumbwe ambaye ni meneja wa msanii Rayvanny.

 

Mazishi ya baba wa Do Fumbwe yamefanyika jijini Tanga. Baadhi ya watu walisikika wakisema kuwa, haiwezekani mtu atembee na walinzi hadi msibani kwani anachoogopa ni kipi?

 

Wengine walisema kuwa, pesa anazowalipa mabodigadi hapo wapatao sita ni bora ingepekwa kama sadaka au rambirambi kwa mfiwa. Mbali na Diamond, wengine wanaotajwa kuwa na tabia kama hiyo ni Harmonize ambaye alifanya hivyo kwenye msiba wa Ruge.


Toa comment