The House of Favourite Newspapers

DIAMOND: Mobeto Siyo Mama Yangu – Video

NADHANI unafahamu kwamba Mei 13 ya kila mwaka, Dunia nzima huadhimisha siku ya wakinamama duniani. Staa wa Filamu Bongo, Mwanamama, Aunt Ezekiel aliitumia siku hiyo kuzindua Short Film yake inayokwenda kwa jina la ‘MAMA’ ambayo ni maalum kwa wakinamama wote kupewa heshima zao kama wazazi, walezi na walimu kwa kwanza katika jamii.

 

Akifanyiwa interview na vyombo vya habari katika uzinduzi huo uliyofanyika usiku wa kuamkia leo, katika ukumbi wa Mlimani City, Diamond alisema asingeweza kwenda na mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa sababu siyo mama yake, hivyo ameambatana na mama yake, Bi. Sandra ambaye amemzaa, kumlea na kumpigania mpaka hapo alipofikia.

Aidha, Diamond Platnumz  alimpongeza Aunt kwa kuandaa filamu hiyo ambayo alisema inaweka wazi thamini ya akinamama wote, ndiyo maana hata amekuwa baba bora kwa kuhakikisha watoto wake wote wanaishi ghorofani.

DIAMOND: “Mobeto Siyo Mama Yangu Siwezi Kuja Nae”

Comments are closed.