Bata la Diamond na Tanasha Usipime!

MPENZI wa staa wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh ameonekana kuweka maneno ya watu pembeni na kuzidi kukolea Kwenye Penzi na Diamond.

Tangu Diamond aweke hadharani kuwa yupo kwenye mahusiano na Tanasha mwaka jana mwishoni ni wazi kuwa hawajapita njia nyepesi kwani Penzi Lao linapingwa sana hasa kwenye Mitandao ya kijamii.

Lakini Diamond na Tanasha wameonekana kupuuzia maneno ya watu na kufanya mambo yao na inaonekana wazi kuwa Tanasha amekolea kwenye Penzi na Mbongo fleva huyo.

Loading...

Toa comment