The House of Favourite Newspapers

Diamond, Zari Walamba Shavu Jarida Maarufu la Sauzi

diamond-m1

Zari na mpenzi wake, Diamond Platnumz,Toleo lijalo la Februari 2017.

MWANAMUZIKI mwenye taito kubwa kwa sasa nchini na Afrika, mtoto wa Tandale na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB), Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenzake, Zarina Hassani ‘Zari’ wamelamba shavu kubwa baada ya kuvuta mkataba wa kupiga picha za kupendezesha jarida maarufu la Afrika Kusini liitwalo ‘Papas and Mamas’.  Kitendo hicho kimewafanyanyote hao  kuingia katika rekodi moja na hayati Nelson Mandela Madiba ambaye naye aliwahi kuandikwa sana katika jarida hilo.

img_20170117_104917_761

Zarina Hassan na Diamond Platnumz, kulia ni Millicent Makhado muigizaji wa filamu nchini Afrika Kusini.

diamond-m

Zarina Hassan ‘Mama Nillan’.

Jarida la ‘Papas and Mamas’ ni maarufu sana Afrika Kusini linalotoka kila mwisho wa mwezi na linaloandika habari za wazazi bora. Mwanzo jarida hili liliitwa ‘Brainchild’ likiwa linamilikiwa na mhariri Nawaal Motlekar likichapwa na kampuni ya Kwenta Media ya huko Afrika Kusini.

mandela1

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela na mjukuu wake Katika Jarida la ‘Mamas and Papas’ Toleo la Julai 2013.

‘Papas and Mamas’ limepatia umaarufu mkubwa baada ya kuandika makala za kuwaelemisha wazazi na kutangaza utamaduni wa Afrika duniani, ikiwa ni pamoja na kuandika makala mbalimbali kuhusu rais mweusi wa kwanza wa Afrika ya Kusini, hayati Nelson Mandela Madiba.

lulu-haangala-zambian

Lulu Haangala Mjasiriamali kutoka Zambia, Toleo la Mei 2016.

Vilevile limeyaongoza majarida yote nchini humo kwa kushika namba moja kuhusu kuandika taarifa za maendeleo ya teknolojia na utafiti katika nyanja ya familia, saikolojia ya mtoto na elimu ya utotoni.

Mums and Babies

Diamond ameingia katika rekodi ya Mandela baada ya kuandikwa na jarida hilo kubwa nchini humo. Yeye na Zari Hassan wameonekana kuwa na familia yenye hadhi ya pekee kiasi ambacho jarida hilo limeandika taarifa zao.mamass

Muvhangos Monamonyane, Toleo la Agosti 2016.  

Mara baada ya picha hizo kusambazwa, zimekuwa gumzo kila kona, kitu kinachowafanya watu wengi kulisubiri mitaani ambapo litaanza kutoka mwezi ujao (Februari). Kuhusu mkwanja waliolipwa mpaka kupiga picha hizo bado haujawekwa wazi ila mtu wa karibu na Diamond alisema jamaa amevuta mkwanja mnono.

 

south-african-actor-and-producer-thapelo-mokoena-who-is-enjoying-his-new-role-as-a-first-time-dad

Thapelo Mokoena, muigizaji kutoka Afrika Kusini akiwa na mtoto wake katika jarida la Mama and Papas, Toleo la June 2015.

Comments are closed.