The House of Favourite Newspapers

Diamond, Ommy Dimpoz wazinguana Marekani!

0

diamond (2) Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Mwandishi Wetu

MAPENZI yanatingisha dunia! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia nyota wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuzinguana laivu nchini Marekani, Risasi Jumamosi limevujishiwa na lina mchapo kamili.

Chanzo makini kilichoshuhudia sakata hilo lililotokea hivi karibuni nchini Marekani kulipokuwa na hafla ya utoaji wa tuzo za Afrimma ambapo Diamond alitwaa 3 huku Dimpoz akipata 1, kimenyetisha kuwa, wawili hao walizinguana wakiwa wanataka kuingia kwenye ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya utoaji wa tuzo hizo.

“Walipokuwa wanaingia ukumbini, Dimpoz akakutana na Diamond sasa Diamond akataka kumsalimia ndipo Dimpoz akachomoa na kumpa maneno ya kejeli ambayo yalimkasirisha nusu wazichape.

“Kila mtu alijua jamaa watashikana mashati. Lakini sema ile busara ya haraka iliwajia, hawakufikia hatua hiyo mbaya,” kilisema chanzo.

ommyOmary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

CHANZO CHA BIFU

Kikaendelea: “Unajua Dimpoz alikataa kupokea salamu ya Diamond maana anasema ni mnafiki. Anadai kwamba, Diamond anapokuwa na watu anajifanya hana tatizo na Dimpoz lakini akiwa na marafiki wa Dimpoz huwa anamzungumzia vibaya na wakikutana na Dimpoz anamsalimia kinafiki ndiyo maana mwenzake akamaindi.”

wema (3)Wema Sepetu ‘Madam’

WEMA ATAJWA

Kikizidi kulipambanua bifu la  mafahari hao wawili, chanzo hicho kilidai kuwa, sababu kubwa ya bifu hilo ilianza muda mrefu baada ya Diamond kumhisi Dimpoz anatembea na Wema Sepetu ‘Madam’ ambaye alikuwa mpenzi wake kwa muda mrefu kisha akamwagwa.

“Kumbe Diamond ana kinyongo na mwenzake. Alimwagwa na Wema lakini nafikiri bado moyoni anampenda sana. Sasa alipoona siku chache baada ya kuachana, ghafla mrembo huyo akaonekana katika pozi tata na Dimpoz, akamuwekea bifu pasipo hata kumuuliza kama ni kweli au la,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Tangu hapo, Diamond amekuwa akimsema vibaya Dimpoz kupitia marafiki zake kitu ambacho Dimpoz anakiona ni unafiki kwani hamwambii mwenyewe. Huwezi amini kule Marekani, Diamond alikuwa ndiye aliyetangulia kufika lakini badala ampokee mwenzake ambaye ni mgeni, akampotezea halafu ukumbini akajifanya anamsalimia.”

wemanadiamond (1)WABONGO WAWASHANGAA

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kitendo cha wawili hao kuzinguana ukumbini wakati wanatokea sehemu moja kiliwashangaza Wabongo waishio nchini humo ambao walikwenda kushuhudia utoaji wa tuzo hizo kwani walitegemea wawili hao wangekuwa kitu kimoja.

“Wabongo wenzao waishio Marekani waliwashangaa sana. Hawajui kwamba huku ndiyo walitakiwa kuonesha umoja wao. Kwanza ndiyo wanainuka katika tuzo kubwa halafu wao wanaleta za uswahilini, itawagharimu siku moja,” kilisema chanzo hicho.


ommydimpoznawemasepetu.jpgDIMPOZ AFUNGUKA

Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, mwanahabari wetu alianza kumtafuta Dimpoz ili aweze kutoa ufafanuzi juu ya kile kilichotokea ambapo alipopatikana, alifunguka:

“Daah! Nani kawapa hizo habari? Nyinyi kweli mnajua kunusa. Ni kweli tulipishana na jamaa (Diamond) kule Marekani.

“Lakini si unajua tena… pengine Diamond ana kinyongo chake na mimi sipendi mtu anayeishi kwa vinyongo, ndiyo maana nilikataa salamu yake, yakatokea hayo lakini kimsingi namshukuru Mungu hatukukunjana wala nini.”

DIAMOND SASA

Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kueleza kwa upande wake hazikuzaa matunda kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa alikuwa safarini nje ya nchi.

“Jamaa siyo rahisi kumpata sababu yupo safarini nje ya nchi labda umcheki tena baadaye,” alisema mtu wa karibu na Diamond pasipo kutaja msanii huyo ameelekea wapi.

TUJIKUMBUSHE

Baada ya Diamond kumwagwa na Wema mwishoni mwa mwaka jana, baadaye Februari mwaka huu, picha zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonesha Dimpoz na Wema wakiwa kitandani, hotelini nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini viliandika kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi huku ikielezwa kwamba, uhusiano huo ulikuwepo kwa siri hata wakati Wema akiwa na Diamond.

Hata hivyo, baadaye ikaja kuelezwa kuwa, Wema na Dimpoz walikuwa nchini humo wakitengeneza video ya wimbo wa Dimpoz uitwao Wanjera.

Leave A Reply