The House of Favourite Newspapers

Diamond Platnumz: Zari Ni Hodari Wa Mapenzi

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa kivutio kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuimba kipande cha wimbo  chenye maneno “Zari Hodari wa Mapenzi”.

 

Diamond ambaye alikuwa kwenye mahusiano na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa takribani miaka minne mpaka walivyomwagana mapema mwaka huu, ameibuka na kusifia ujuzi wa mapenzi wa mama watoto wake huyo.

 

Diamond amesema maneno hayo kupitia kipande cha video kilichomwonyesha akiimba wimbo mpya wa msanii kutoka WCB,  Mbosso,  uitwao ‘Hodari’ ambapo ndani yake amemtaja Zari kama hodari wa mapenzi.

Comments are closed.