The House of Favourite Newspapers

Diamond, Rayvanny, Nandy Washinda Tuzo za Marekani

STAA wa Bongo Fleva, nasbu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ameshinda tuzo mbili za African Entertainment Awards USA 2018 zilizofanyika juzi Jumamosi, Oktobea 20, mjini New Jersey nchini Marekani.

Diamond ameshinda kwenye vipengele vya Best Collaboration Of the Year kupitia wimbo wake wa African Beauty ambao amemshirikisha msanii wa Marekani, Omarion. Mbali na tuzo hiyo, Diamond pia ameshinda kipengele cha Best Male Artist of the Year.

 

Mwanamuziki mwingine kutokea WCB, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ amefanikiwa Kushinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha ya Best Vocalist of the Year.

 

Msanii mwingine wa Bongo ni Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ambaye ameshinda kipengele cha Best Single Female kupitia wimbo wake wa Kivuruge.

 

Mbali na wasanii hao, DJ wa Diamond Platnumz ambaye pia ni kaka yake, Rommy Jones ameshinda kwenye kipengele cha Best Dj of the Year.

MASHAKA AFARIKI: Muhogo Mchungu afunguka kila kitu

Comments are closed.