The House of Favourite Newspapers

Diamond: WASAFI FESTIVAL Kurudiwa Bure leo Sumbawanga – Video

Tamasha la Wasafi Festival lililokuwa likifanyika jana (Jumamosi) usiku limeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha na hivyo kushindwa kuendelea.

Hata hivyo onesho hilo lililokuwa likifanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa liliahirishwa huku wasanii Country Boy, Queen Darlin, Gigy Money, Lavalava na Young Killer (pichani kwenye machela) wakiwa tayari wameshamaliza kupiga shoo zao jukwaani.

Kutokana kuahirishwa kwa tamasha hilo Msanii Diamond Platnumz alipanda jukwaani na kuwaomba radhi mashabiki waliokuwa uwanjani hapo na ambapo alitangaza kuwa Tamasha hilo litaendelea tena uwanjani hapo leo Jumapili jioni kuanzia saa 10:00.

Wasanii wote ambao hawakufanya makamuzi usiku wa kuamkka leo sababu ya mvua hizo, watapanda jukwaani leo Jumapili kukamua kama kawa.

PICHA : RICHARD BUKOS /GPL  – SUMBAWANGA

Comments are closed.