The House of Favourite Newspapers
gunners X

Diamond, Wema Siyo Siri Tena

0

WEMA

MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse amemwaga ubuyu kwamba, kuna kila dalili Diamond na Wema wakawa wamerudiana kwani siyo jambo la siri tena.

 

Maimartha anasema wawili hao walikula kiapo cha damu hivyo ni ngumu kuachana moja kwa moja na kila mtu ana hamu kuwaona Diamond na Wema wakiwa wameoana.

Ukubwa wa majina yao uliwafanya watu wengi kuwa mashabiki na wafuatiliaji wakubwa wa mapenzi yao. Kipindi hicho vyombo vya habari mbalimbali story kubwa ilikuwa ni kuhusiana na uhusiano wao wa kimapenzi.

 

Hasa @diamondplatnumz alipita kwa @zamaradimketema na hapa anaelezea sababu zilimpelekea kuvunja mahusiano na mrembo Wema Sepetu. Lakini Diamond na Wema Sepetu wana historia ya kuachana na kurudiana.

Mara kwanza @wemasepetu kukubali hadharani kuwa yeye na @diamondplatnumz ni mpenzi wake ilikuwa mwaka 2012. Wema anasema… “He is Dark and Chocolate, Dresses Good, smells Good”

 

Pia walikuwa na Plan ya kufungua kampuni yao ambayo ingeitwa #DW na ingejihusisha masuala ya Music & Movies, kwa sababu @wemasepetu ni Actress mkubwa nchini, na @diamondplatnumz pia hivyo hivyo msanii mkubwa nchini Tanzania 🇹🇿

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply