The House of Favourite Newspapers

Diamond, Wizkid Vita ya Kikubwa

0

MAJINA ya wanamuziki mbalimbali yametajwa kuwania Tuzo za MTV EMA 2021 ambazo zitafanyika jijini Budapest nchini Hungury katika Bara la Ulaya mwishoni mwa 2021.

Hata hivyo, vita ya kikubwa imejitokeza kwa mara nyingine ambapo staa wa muziki wa Tanzania, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz amegongana kwa mara nyingine kwenye kipengele kimoja na Wizkid wa Nigeria.

Katika listi hiyo, Diamond ndiye mwanamuziki pekee anayeiwakilisha Afrika Mashariki na Kati.

Diamond ametajwa kwenye Kipengele cha Best African Act ambapo anachuana na wakali wengine kutoka Afrika kama Wizkid Tems, Burna Boy, Focalistic na Amaarae kutoka nchini Ghana.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 14, 2021 ambapo mwanamuziki Justine Bieber ameongoza kwa kutajwa kwenye kuwania vipengele vingi ambapo ametajwa katika vipengele nane.

Ukiacha tuzo hizo za MTV EMA, pia jamaa hao wanaumana kwenye Tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) 2021 ambapo Diamond, Wizkid na Burna Boy wapo vitani.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply