DIAMOND: ZARI ALIKUWA AKI-DATE NA PETER WA P SQUARE

STAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz,  ameanika sababu za kuachana na kutorudiana na mpenzi wake ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Zari The Boss Lady,  nayeishi nchini Afrika Kusini kwa sasa na watoto hao.

 

Akizungumza wakati wa mahojiano na Wasafi FM jana Aprili 23, 2019 usiku, Diamond alisema:

 

“Namheshimu Zari ni mzazi mwenzangu, alikuwa wife material, alikuwa anatoka na Peter wa P Square, niliwahi kukuta sms nikamuuliza, alikuwa anachepuka pia na ‘trainer’ wake na alikuwa anamleta hadi kwangu, lakini sijawahi kufunguka, na ukweli sijawahi kuachwa na mwanamke, ukizingua nitakupiga matukio utaondoka mwenyewe.

 

“Mpaka nyumbani kwangu na mpaka picha pia ninazo ila mimi sio mtu wa kujifanya, mimi siongei mpaka naulizwa kwa nini sizungumzi,  na kiukweli licha ya mambo yote hayo labda mimi nilikuwa ni chanzo kwa sababu mimi nilikuwa mwendawazimu kwelikweli na yeye alikuwa ananipenda sana ila mimi nilikuwa nampenda lakini sio kama yeye alivyokuwa ananipenda mimi”.

 

 

Loading...

Toa comment