Diamond, Zari Motomoto

 

KILA moto wa penzi la Diamond na Zari unapotaka kuzima, ni kama kuna mtu anauwekea mafuta na mambo yanakuwa fayafaya.

 

Stori mpya kwa wawili hao ambao wamefanikiwa kuzaa watoto wawili ni kwamba, mtandao wa Netfflix tawi la  Afrika Kusini umetangaza kuwa, utarusha makala (documentary) yao hivi karibuni iliyopewa jina la ‘Young, Famous & African’.

 

Hivi karibuni Netflix ilimpa shavu Indriss Sultan la kushiriki filamu ya Slay na kuonekana kwenye mtandao huo unaojihusisha na masuala ya Filamu duniani kupitia mitandaoni.

 

Kitendo cha mtandao huo kuanza kurusha makala za Diamond na Zari kinatajwa kuamsha upya “kelele” za wawili hao mitandaoni ambao wamekuwa wakipigiwa msasa na mashabiki zao kuwa kapo yao inawavutia na hivyo kuwataka waoane yaishe.

 

Baada ya kupatikana kwa taarifa hiyo ya Netflix, Zari ni kama alimeza asali ambapo haraka aliwataka mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kukaa mkao wa kula kuisubiri ‘siriz’ ya makala yake na mzazi mwenzake.


Toa comment