DIANA KIMARI: WEMA HAJANIBADILI TABIA

Diana Kimari

MSANII wa filamu Bongo, Diana Kimari amefunguka kuwa mwigizaji Wema Sepetu hajambadilisha tabia kama baadhi ya watu wanavyosema mitandaoni.  

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Diana alisema watu wengi wanahoji kuhusu ule ukaribu wake na Wema kuwa haukuwa wa kawaida, huku wengine wakiongeza kwamba alikuwa anasali lakini tangu alipoanza kuwa karibu na staa huyo ameacha kitu ambacho amesema hakina ukweli.

 

“Unajua zamani nilikuwa naposti sana mambo ya kanisani kwenye akaunti yangu, lakini mambo yalikuja kubadilika baadaye nikaona hakuna umuhimu tena wa mimi kuendelea kuposti kila kitu changu mtandaoni, hivyo watu wakadhani nimeacha kusali kitu ambacho si kweli, kutoposti hivyo vitu haimaanishi kwamba nimeacha ulokole wangu.

“Pia mimi ni mdogo sio mkubwa kihivyo kwa hiyo mpaka sasa bado nipo chini ya uangalizi wa wazazi wangu hata kipindi naishi kwa Wema wazazi wangu walikuwa wanajua, kwa hiyo hawatakubali wanione naharibikiwa wakati wao wapo hai, wananichunga sana yaani sijui nisemaje,” alisema Diana.

STORI: Memorise Richard

Toa comment