DIANA SASA YEYE NA MUNGU TU

 

Diana Kimari

 TUMRUDIE Mungu! Mwigizaji mwenye mbwembwe lukuki Bongo Muvi, Diana Kimari ameweka wazi kuwa kuna kila sababu kwa mastaa kumpa nafasi Mungu kama anavyofanya yeye.  

 

Diana aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa anashangazwa na mastaa wengi kutokuwa karibu na Mungu kwani wanaoamka Jumapili na kwenda kazini anawajua ni wachache mno, jambo ambalo siyo sahihi.

 

“Hakuna kitu kibaya kama kama kujisahau kuwa ni muhimu kuwa na uhusiano mzuri na Mungu maana mastaa wengine wanaweza kumaliza hata miaka hawajakanyaga kanisani, sasa filamu zetu zinawezaje kusonga mbele wakati hatumpi nafasi aliyetuumba?” Alihoji Diana.


Loading...

Toa comment