DIANA: SEMENI ILA KWA WEMA NIMEFIKA !

Diana Kimari

MUIGIZAJI Diana Kimari amesema kitendo cha yeye kuwa na urafiki wa karibu na Wema Sepetu kimeibua maneno mengi mitandaoni lakini kamwe maneno hayo hayawezi kumfanya aache kumpenda shosti wake huyo.

Akizungumza na Amani, Diana alisema kuwa Wema amekuwa zaidi ya dada kwake na ni mtu mwenye roho ya kipekee sana hata waseme vipi habanduki kwake. “Najua kuna watu wengi sana hawapendi kuniona na Wema, yule ni zaidi ya dada kwangu yaani sijaona mtu mwenye roho ya kipekee kama yeye kiufupi nampenda wanaojaribu kuleta fitina watagonga mwamba tu,” alisema Diana.

 

Wema amewahi kuwa na ushosti na warembo kibao akiwemo Snura Mushi, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na wengineo lakini hata hivyo, kwa nyakati tofauti ukaribu wao ulikufa bila kufahamika sababu

Stori: Imelda Mtema

Loading...

Toa comment