The House of Favourite Newspapers

Diana: Simchukii Mobeto, Ila Wema Mapenzi Kama Yote

MWIGIZAJI wa Bongo Muvi mwenye vituko lukuki, Diana Kimari amefunguka kuwa watu wengi wanasema ana bifu na mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa sababu yupo karibu na Wema Sepetu, jambo ambalo si kweli bali ana mapenzi kama yote kwa Wema.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Diana ambaye hivi sasa yupo karibu na Wema alisema watu wengi wanajua ana bifu na Mobeto, lakini wanashindwa kuelewa anapoweka vitu vyake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram havilengi kumsema mtu.

“Simchukii na wala sina tatizo na Hamisa (Mobeto) kama watu wanavyotengeneza kwenye mitandao, bali wakiona namuweka Wema ni kwa vile nina mapenzi kama yote kwake pia hata nikiandika ujumbe simsemi mtu,” alisema Diana ambaye alifanya vizuri kwenye Sinema za Family Disaster, Kigodoro na nyinginezo.

MAMA Diamond Akataa Kutaja Zawadi ya Wema/ Atumwa na Diamond?

Comments are closed.