The House of Favourite Newspapers

Diarra Aipa Jeuri Yanga Ligi Kuu

0

UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa uwepo wa kipa raia wa Mali, Djigui Diarra umemaliza tatizo kubwa katika kikosi hicho.

 

Kipa huyo ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo msimu huu akichukua nafasi ya Metacha Mnata aliyetimkia Polisi Tanzania.

Kipa huyo tangu amejiunga na Yanga, ameruhusu bao moja ndani ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wakati Yanga ikishinda 3-1.

 

Amecheza mechi tano, ana clean sheet nne.Akizungumza na Spoti Xtra, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, alisema siyo kitu kidogo kumsajili kipa aliyekuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Mali.

 

Said alisema kwa hivi sasa hawafikirii suala la kipa na badala yake wanaangalia nafasi nyingine muhimu katika kukiboresha kikosi chao.

 

“Misimu iliyopita tulikuwa na tatizo la golikipa kutokana na upungufu kadhaa waliokuwa wanaufanya makipa wetu.“Lakini msimu huu hatuyaoni mapungufu hayo tangu Diarra alipojiunga na Yanga ambaye yeye ndiye anayeichezesha timu kwa kuanzia golini.“Ubora wake ameuthibitisha katika michezo mitano mfululizo ya ligi ambayo ameicheza kwa kuruhusu bao moja pekee, Diarra ni kati ya makipa wanne wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Mali,” alisema Said.

Leave A Reply