Diarra Ashusha Bonge la kipa Yanga

UPO uwezekano mkubwa wa Yanga kushusha kipa mwingine mwenye uwezo mkubwa kama Djigui Diarra raia wa Mali.Djigui alijiunga na Yanga msimu huu baada ya timu hiyo kuachana na Farouk Shikalo na Metacha Mnata. Mbali na Diarra, Yanga pia ilimsajili Erick Johora.

 

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, timu hiyo inataka kumsajili kipa huyo atakayechukua nafasi ya Diarra ambaye atakuwepo katika kikosi cha Mali kitakachocheza michuano ya AFCON mwakani nchini Cameroon.

 

Bosi huyo alisema kuwa, kipa huyo huenda akawa mzawa mwenye kiwango kikubwa, huku akifichua kwamba, lengo la kusajili mzawa ni kutoa nafasi ya kusajili kiungo na straika wa kimataifa.

“Huenda Yanga tukasajili kipa mmoja mzawa mwenye kiwango bora atakayekuwa mbadala wa Diarra.“Hiyo ni kutokana na kipa huyo kukosekana katika michezo ya ligi kutokana na kubanwa na majukumu ya timu ya taifa ya Mali.

 

“Hivyo Kamati ya Mashindano inajadiliana katika kumpata mbadala wa Diarra kwa kipindi ambacho hatakuwepo na timu,” alisema bosi huyo. Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, hivi karibuni aliliambia Spoti Xtra kwamba: “ Tumepokea mapendekezo ya kocha wetu ambayo ni siri, hivi karibuni tutaweka wazi.”

STORI: MUSA MATEJA NA WILBERT MOLANDI


Toa comment