The House of Favourite Newspapers

Diarra, Bigirimana Watimka Yanga, Kuwakosa Singida leo, Kaze Athibitisha

0
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze.

 

YANGA SC imethibitisha kuwakosa wachezaji wake watatu, Djigui Diarra, Gael Bigirimana na Stephane Azzizi Ki kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Singida Big Stars unaotarajiwa kufanyika leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Yanga itaingia ikiwa na rekodi bora ya kucheza mechi 46 mfululizo za ligi bila ya kupoteza.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, aliweka wazi juu ya kuwakosa wachezaji hao akisema Diarra na Bigirimana wanaenda kuzitumikia timu zao za taifa, huku Azizi Ki akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu ambapo tayari amekosa moja dhidi ya Kagera Sugar.

Djigui Diarra

 

“Diarra na Bigirimana wameitwa kwenda kwenye majukumu ya timu zao za taifa, wakati Azizi Ki akiendelea kuitumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu, huu ukiwa ni mchezo wake wa pili kutumikia adhabu hiyo.

 

“Kwa upande wetu tumefanya matayarisho kutokana na ukubwa wa mpinzani wetu ambao tunafahamu wana timu nzuri, malengo yetu ni kushinda na tunaamini tunakwenda kupata matokeo mazuri,” alisema kocha huyo.

 

Kwa upande wa Kocha wa Singida Big Stars, Hans van der Pluijm, alisema: “Ninafurahi nakwenda kukutana na timu yangu ya zamani, Yanga ni kama nyumbani kwangu, naamini itakuwa vema kukutana nao tena lakini nikiwa na timu nyingine.

 

“Tunaheshimu wana timu nzuri, lakini sisi tupo tayari kwa ajili ya kupambana nao ili kupata matokeo mazuri.”

STORI NA MARCO MZUMBE

Leave A Reply