DIDA AZUA GUMZO UKUMBINI

HUYU naye! Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Redio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ amegeuka habari na kuwa gumzo ukumbini.  Dida aligeuka gumzo hivi karibuni mkoani hapa katika shughuli ya bethidei ya mdogo wake, Warda Makongwa ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Planet FM ya mjini hapa.

Katika sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Tanzanite uliopo Msamvu mkoani hapa, Dida alikuwa mmoja wa mastaa ambaye aligeuka kuwa gumzo kutokana na matukio aliyokuwa akiyafanya.

Kwanza kabisa, Dida alitinga ukumbini hapo saa 6:00 usiku huku akiwa amevaa kigauni kifupi kilichomwacha wazi sehemu ya mapaja yake. Baada ya kuingia, moja kwa moja alipanda stejini na kuanza kucheza kihasarahasara huku kigauni hicho kikipanda na kuacha wazi sehemu zake nyeti.

Wakati burudani ikiendelea kutolewa na Kundi la Baikoko kutoka jijini Tanga, Dida alijikuta akipagawa na kucheza kwa staili ya kuinama ambapo kigauni chake kilipanda juu na sehemu zake nyeti kubaki wazi.

Hali hiyo ya kuacha nje nyeti zake hizo iliibua minong’ono kutoka kwa wageni waalikwa wanaojiheshimu wakisema kuwa alichofanya siyo sawa. “Huyu Dida ni mtangazaji mwenye jina kubwa nchini, kwa mantiki hiyo ni kioo cha jamii, lakini mavazi na matendo yake anayofanya hapa ukumbini ni kinyume na maadili,” alisikika mgeni mmoja wa wageni waalikwa akijadiliana na mwenzake.

AONYESHA JEURI YA FEDHA

Licha ya kumwaga lazi huko, Dida alizua gumzo jingine baada ya kuonesha jeuri ya fedha ambapo alinunua kreti nyingi za bia na kugawa kila meza kreti mojamoja huku akiwaamuru mabaunsa kufunga mageti yote ili watu wasitoke nje mpaka wamalize vinywaji hivyo.

Gumzo halikuishia hapo, liliendelea kutokana na mtangazaji huyo kuketi kwa muda mrefu na mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa hereni na amebeba mikoba ya kike. Alipofuatwa na mwandishi wetu kujua kulikoni ‘kufyetuka’ kiasi hicho, Dida aliomba atafutwe siku nyingine kwani hakuwa tayari kwa mahojiano.

STORI: DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO

Toa comment