The House of Favourite Newspapers

Difenda Mbili Zamlinda Morrison Dar

0

ULINZI mkubwa ulitawala jana kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison akisubiria hukumu yake.

Hiyo ikiwa ni siku ya pili tangu kiungo huyo afikishwe kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za mkataba wa kuitumikia timu hiyo ndani ya jezi nyekundu.

Kamati hiyo ilikutana juzi asubuhi na kufanya kikao kizito ambacho kilianza juzi Jumatatu asubuhi na kumalizika usiku, lakini hakikutoa majibu na jana walikutana tena kuanzia asubuhi.

 

Hata hivyo, kulikuwa na ulinzi mkali sana baada ya difenda mbili zikiwa zimejaa askari kuingia eneo hilo ambapo moja ilidumu kwa muda mchache na kuondoka, Wachezaji ya TFF kutokana na matatizo yaliyoonekana kwenye mkataba wake na Yanga.

 

Awali ilielezwa kuwa Morrison alisaini mkataba wa miezi sita na timu hiyo, lakini wakati inaelezwa kuwa anaweza kujiunga na Simba, Yanga walisema kuwa wamempa mkataba wa miaka miwili.

 

Hata hivyo, kabla ya kumalizika kwa sakata hilo, Simba waliweka picha ya kiungo huyo kwenye mtandao wao akiwa anasaini ambapo nyingine ilikaa hapo kwa saa tatu na kuwashusha baadhi ya askari na kuondoka.Hii ni mara kwanza ulinzi mkali zaidi unaonekana kwenye shirikisho hilo wakati kamati hiyo ikiwa inakaa kujadili jambo lolote linalohusu mchezaji.

 

Hakuna mtu yeyote ukiachana na viongozi wa kamati hiyo au wale wa TFF ambao walikuwa wanaruhusiwa kusogea karibu na geti la ofisi hizo jana, sehemu ambao ilikuwa na walinzi ambao siku zote wanalinda kwenye geti hilo

 

Kiungo huyo jana alifika kwenye shirikisho hilo saa saba mchana na moja kwa moja kuingia katika ofisi hizo, tayari kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo ambayo ilikaa hadi saa 10: 10 jioni.Baada ya hapo askari walitoka na kuwaondoa mashabiki wote waliokuwa wamejazana nje ya geti hilo.

Stori: Joel Thomas na Said Ally

Leave A Reply