The House of Favourite Newspapers
gunners X

Dili la Ajibu Kusepa Simba, Majibu Yapo Hapa

0

BAADA ya hivi karibuni kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu kudaiwa kupata dili la kuwaniwa na moja ya timu kutoka nje ya Tanzania, uongozi klabu yake unadaiwa kuwa tayari kumruhusu kuendelea na maisha yake mengine nje ya kikosini hapo.

 

Imeelezwa kuwa Ajibu amepata dili hilo lakini maambukizi ya Virusi vya Corona yamekuwa kikwazo kwake kukamilisha mchakato wa mazungumzo ya usajili, hivyo inasubiriwa janga hilo limalizike ili kila kitu kiendelee.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi mmoja wa viongozi wa Klabu ya Simba alisema kuwa uongozi wao umefikia hatua hiyo kwa sababu Ajibu hana jambo lolote kubwa alilolifanyia Simba tangu ilipomsajili mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga.

“Kama amepata timu ya kucheza nje ya nchini sisi hatuna kizuizi, hatuwezi kumzuia.“Tangu atue katika kikosi chetu hajafanya jambo kubwa sana na amekuwa akipata wakati mgumu katika kikosi cha kwanza, kama kuna timu ameoata ije tutazungumza vizuri tu,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe kuwa kuwa siyo msemaji wa klabu.

 

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ili azungumzie hilo hakupatikana.Upande wa Meneja wa Ajibu, Rahim Abbas alisisitiza kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo na lingine lolote kwa kuwa afya yake haiko vizuri.

Leave A Reply