The House of Favourite Newspapers

DILI ZA ZARI BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ USIPIME

Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’

FEBRUARI 14, mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ itaendelea kuwa kumbukumbu kwa mwanamama mjasiriamali ambaye pia ni msanii, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ baada ya ‘kufumba macho’ na kuamua kuachana rasmi na mzazi mwenzake ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Zari amezaa na Diamond watoto wawili, Latiffah na Nillan na kabla ya kuachana kwao, alikuwa akipata madili ‘mikataba’ iliyowajumuisha wote kama vile ya maduka ya nguo, mitandao ya simu pamoja na benki, lakini tangu wameachana amekuwa akila dili nono kibao peke yake. Over Ze Weekend imeingia chimbo na kuibuka na dili zake zote alizoziweka kwapani tangu aachane na Diamond;

UBALOZI WATOTO

Lilikuwa zali la kwanza siku chache baada ya Zari kutua Dar akitokea kwenye makazi yake, Afrika Kusini ‘Sauz’. Zari alisaini dili la kuwa balozi na kutangaza ‘pempas’ za watoto, Soft Care na kuzua gumzo kwa mastaa Bongo ambapo mashabiki wengi walicharuka iweje mtu wa nje ya nchi aje kulamba mkataba kirahisi huku mastaa wa Kibongo wakiwa bize mitandaoni.

MISS UGANDA

Siku chache baada ya dili hilo, Oktoba 10, Zari alilamba dili lingine la kuwa miongoni mwa majaji katika usiku wa Miss Uganda 2018 uliofanyika ndani ya Hoteli ya Kampala Sheraton.

BALOZI WA WATOTO

Akiwa bado nchini Uganda ambapo ndipo alipozaliwa, Zari alipata shavu la kuwa balozi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Brayan White Foundation ambapo atakuwa akishirikiana nao kwa ukaribu.

UBALO-ZI WA UTALII

Madili hayo hayakuishia hapo, mwishoni mwa Septemba, mwaka huu Zari aliitwa na Wizara ya Utalii na Wanyama nchini Uganda. Kuonesha ‘usiriazi’ na dili hilo, Zari aliingia katika wizara hiyo na kuonana na waziri wa Utalii, Godfrey Kiwanda na kufanya mazungumzo naye. Ubalozi huo, unamfanya kutumia nguvu ya mitandao yake ya kijamii katika kuutangaza utalii wa Uganda ndani na nje ya nchi.

KUTANGAZA MAJARIDA

Dili lingine alilolamba mjasiriamali huyu ni kupata nafasi ya kutangaza jarida la Kenya ambalo linapatika Afrika Mashariki lijulikanalo kama True Love ambapo alishapamba katika ukurasa wa mbele na kuuza nakala kibao.

MC NA BABA WA BEYONCE

Shavu hili lilikuwa hivi karibuni nchini Afrika Kusini ambapo kwa mara ya kwanza alikutana na meneja wa vipaji ambaye pia ni baba wa staa wa R&B, Beyonce Knowles, Dk Mathew Knowles. Wawili hao walikutana baada ya Zari kupata dili la kuwa MC sambamba na baba huyo katika tuzo maalum za 2018 African Leaders 4 Change.

NEEMA ADRIAN

Comments are closed.