The House of Favourite Newspapers

Dilunga Achekelea Ofa ya Yanga

Hassan Dilunga

KIUNGO aliyewahi kupigwa chini na Yanga kwa madai kwamba amechuja, akatua Mtibwa Sugar na kung’ara, Hassan Dilunga yuko tayari kurudi Jangwani.

Mchezaji huyo bora wa mashindano ya Kombe la FA, amesema kuwa ni jambo la furaha sana kwake kutakiwa na timu kubwa kama Siginda United na Yanga.

 

“Kwangu mimi ni jambo la faraja kuwa na mazungumzo na timu za Ligi Kuu hivyo sina mashaka na hilo kwani kazi yangu mimi ni mchezaji na ninapohitajika kutumikia timu nyingine maana kuna kitu cha pekee ambacho timu inayohitaji huduma yangu imekiona hivyo sina chaguo na kazi.

 

“Timu zote ambazo nimekuwa nikihusishwa kujiunga nazo ambazo ni pamoja na Yanga, Singida United nimewaweka wazi kwamba nina mkataba na timu yangu ya Mtibwa hivyo kama kweli wanahitaji huduma yangu wazungumze na uongozi kisha nami nitasaini timu yoyote ambayo itakuwa ina maslahi mazuri kwangu,” alisema Dilunga ambaye amewahi kucheza JKT Ruvu.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA, DAR ES SALAAM

Comments are closed.