The House of Favourite Newspapers

Dilunga: Sevilla watanipeleka Ulaya

KIUNGO wa Simba, Hassan Dilunga amesema ujio wa klabu ya Sevilla hapa nchini utatimiza ndoto yake ya kwenda Ulaya kucheza soka la kulipwa.

 

Dilunga amesema alikuwa na ndoto za kwenda Ulaya kucheza soka katika timu kubwa, hivyo anaamini ujio wa Sevilla inayotoka kwenye ligi ya La Liga ambayo ni kubwa duniani, itafungua njia ya kwenda Ulaya kutimiza ndoto zake.

 

Sevilla wanatarajiwa kutua nchini wiki ijayo kufanya ziara ya kimichezo na watacheza mchezo wa kirafi ki dhidi ya klabu ya Simba utakaopigwa Mei 23 kwenye Uwanja wa Taifa. Dilunga aliliambia Championi Jumatano kuwa, anashukuru kupata nafasi ya kucheza na Sevilla kwa kuwa anaamini ndoto yake ya kwenda Ulaya inakuja kutimia kwani atautumia mchezo huo kama daraja la kuonekana na timu zingine kubwa.

 

“Ndoto yangu siku zote ilikuwa ni kwenda Ulaya kucheza soka la kulipwa, hivyo ujio wa Sevilla hapa nchini nitautumia kama daraja la kwenda nje ya nchi na kutimiza ndoto yangu ya muda mrefu,” alisema Dilunga.

Comments are closed.