DIRISHA HALIFUNGWI NA KUFULI

SHOGA shangaa-shangaa mjini hapa, kama ni msimu embe subiri mwisho wa mwaka ndiyo hizooo zaja, uongo? Ukitaka kujifunza mbio wanasema mchokoze chizi, haloooo eeeehh! Utajibeba mwaka huu wakati mbeleko zinafungwa kiunoni wajanja wanachezea vigodoro, upo nyonyo? 

 

Asikwambie mtu, kona hii inawafunza wengi, hizo simu na meseji ninazopata kwa siku shoga, utadhani wameambiwa miye ndiye mganga wa kienyeji sijui, heeee heeeiyaaa! Weee naweee, bati bovu la nini kwenye chumba cha honeymoon?

 

Shoga, leo nipo na walee akina mama ambao wanashindwa kabisa kuhifadhi vitu vyao kwenye makoromeo, kucha kuwashirikisha majirani, utakuta jirani anamjua mwenzake kama ugonjwa wa ukoma! Anajua leo wamekula nini asubuhi, mchana, usiku na hata kile chakula cha usiku na mumeo jirani anajua hadi staili walizopeana, shuuuutuuuuu! Hivi ninyi wanawake niwafunze vipi mjue utu na thamani yenu! Sawa hivyo vilongalonga sijui vya kupangusa ndiyo vimewafanya kila kitu kuambiana kwa haraka! Sawa, hatukatai jirani yako ndiye atakayekuzika, lakini siyo kila kitu ajue basi!

Chefuuuuuu!

Utakuta mama mtu mzima na watoto wanne juu lakini anamshirikisha jirani yake kila kitu kinachomhusu ndani hadi jirani akimuona mume wake anakuwa amemjua nje ndani ya zipu yupoje! Kesho na keshokutwa kama humridhishi kisha huyo jirani akakuzunguka na kutembea naye ukajua utasema mchawi nani kama siyo mwenyewe, limbukeeeeeniiii!

Shoga wanakwambia ukitaka kujua umuhimu wa maji ya msalani ndoo itoboke! Siyo kila kitu jirani ajue, kuna maisha unatakiwa kuyakwepa, utakuta umeshinda na njaa jirani anajua, mumeo hana pesa au kashindwa kukuridhisha jirani anajua, aliyekwambia huyo jirani hana wivu ni nani? Kuna wengine sasa, bila hata tone la aibu, kutwa kushinda kwa jirani yake, atakula, atakalia hayo masofa hadi kuingia chumbani kwa mwenzake kujipodoa, kuondoka kwake sasa, mpaka mumewe arudi kutoka kazini, hooovyooo!

 

Wakati mwingine huwa najiuliza hivi sisi wanawake ujasiri mwingine kama huu huwa tunatoa wapi? Kwa nini hatuna hata shipa la aibu! Ina maana mwalimu wetu siye bado ni kipofu hadi leo jamani? Shoga, ifike mahali basi tuwe tunajifikiria mara mbilimbili, tabia zako za nyumbani siyo vizuri jirani yako azijue, kama hukutandika kitanda, mmelala na njaa, tabia za mumeo hizo ni siri zako.

 

Neno langu siyo sheria, lakini zingatia shoga, tangu lini dirisha likafungwa na kufuli? Jirani yako mwisho sebuleni na siri nyingine zibaki kwako na familia yako! Kwa leo sina mengi shoga, kwa maoni na ushauri usisite kunitafuta kwa meseji, namba zangu hizo hapo juu.

Ni mimi Shangingi Mstaafu, Anti Nasra wa Ukwee

JAMAA Aliyejifanya ‘MCHUNGAJI’ Alivyokamatwa na Madawa DAR!


Loading...

Toa comment