The House of Favourite Newspapers

Ditto afungukia Moyo Sukuma Damu

moyo-sukuma-damu-3

ANDREW CARLOS

MMOJA kati ya wakongwe wa Muziki wa Bongo Fleva, Lameck Ditto ameifungukia ngoma yake ya Moyo Sukuma Damu kuwa ni sanaa tu na wala haijamlenga mtu yeyote.

moyo-sukuma-damu-11Akizungumza na Global Publishers, Ditto aliyewahi kuwika na vibao kibao ikiwemo Tushukuru kwa Yote na Moyo wa Subira alisema kuwa, Moyo Sukuma Damu ilikuwa moja ya hisia zake katika kuandika mistari na alihitaji ‘engo’ itakayomsaidia kufikisha ujumbe aliokusudia.

moyo-sukuma-damu-1“Nilikaa chini nikafikiri mara nyingi, haikuwa rahisi au kazi ya mara moja. Nikiwa nimeshaandika mistari kadhaa likanijia wazo la kuukumbusha moyo majukumu yake ndipo nikaita jina la Moyo Sukuma Damu,” alisema Ditto ambaye kwa sasa ni nguzo katika Jumba la Vipaji (THT).

Comments are closed.