The House of Favourite Newspapers

Ditto: Moyo Sukuma Damu ni ‘Idea’ ya Miaka Miwili

lameck-ditto-1

Msanii wa kizazi kipya anayesumbua kwa sasa na ngoma yake mpya ya Moyo Sukuma Damu, Lameck Ditto leo katika mahojiano na Global Tv Online, amefunguka kuwa idea ya wimbo huo aliihifadhi kwa miaka miwili kichwani.

lameck-ditto-2Lameck Ditto akiwaStudio za  Global TV Online.

“Nilikuta washkaji wanapiga stori na kwa malumbano kidogo, nikategea sikio kusikia malumbano yale yalikuwa ni ya jambo lipi? Kusikia moyo na mapenzi nikasogea jirani nipate japo kitu kipya maana walionekana kuwa smart sana wale jamaa, basi nikasikia kazi ya moyo hadi waka-google kuangalia kazi ya moyo na kundi lililoshinda malumbano lilikuwa ni lile lililosema moyo kazi yake ni kusukuma damu na mengine ni ziada tu,” alisema Ditto.

Hapo ndipo lilipozaliwa wazo la wimbo huu na kazi iliyokuwa imesalia ni kuandaa melody, midundo na mashairi tu.

Miaka miwili baadaye Ditto alikwenda kwa Emma The Boy, alikuta mdundo upo tayari na kilichokuwa kimebaki ni mashairi na melody tu. Alitumia muda mfupi sana na wimbo ulirekodiwa mara moja. Hii ni kutokana na uzoefu waliokuwa nao Ditto na Emma wakati wa kurekodi.

 

 

Salum Milongo/GPL

 

 

 

 

 

Comments are closed.