The House of Favourite Newspapers

Diwani Mkuranga Awaliza Wananchi Wake Kwa Furaha

0
Diwani wa Kata ya Mkuranga mkoani Pwani, Shabani Manga mwenye (koti) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Tegelea.

PWANI: 2 Machi 2023, Diwani wa Kata ya Mkuranga mkoani Pwani, kupitia Chama cha Mapinduzi, Shabani Manga, jana (Jumatano) alizindua zahanati katika Kijiji cha Tegelea ambapo uzinduzi huo ulihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi wa kijiji hicho.

Dokta Yasir ambaye ni mwanzilishi wa ujenzi wa zahanati hiyo akizungumza kwenye hafla hiyo.

Katika tukio hilo baadhi ya wananchi walionekana wakibubujikwa na machozi ya furaha kwa kujengewa zahanati hiyo kijijini hapo.

Mmoja wa wanakijiji waliokuwa kwenye uzinduzi huo alisikika akisema hapo awali kinamama waliokuwa wakitaka kujifungua walikuwa wanapata taabu sana kupata huduma ya dhararu unafikia wakati wa kushikwa na uchungu lakini sasa wamekombolewa.

Ahmed Salum Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Wilaya na Mkoa Chama cha Mapinduzi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo.

Akizungumza na wananchi waliofurika kwenye uzinduzi huo, diwani Manga aliwaambia kuwa zahanati hiyo kuanzia sasa ni mali ya kijiji hicho na imesajiliwa kihalali kabisa na ni wajibu wao kuitumia na kuitunza.

Aidha diwani Manga alimpongeza Mganga aliyemtaja kwa jina la Dokta Yasri kwa uzalendo wake ambaye ndiye aliyeanza ujenzi wa zahanati hiyo kwa nguvu zake binafsi na marafiki zake kabla ya serikali kutia mkono wake na kuimalizia. Alisema diwani Manga kwenye uzinduzi huo.

Wengine waliozungumza kwenye mkutano huo ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya wilaya na mkoa wa Pwani, Ahmed Salum ambaye aliwasisitiza wananchi kuendelea kuwa na imani na chama hicho kama wanavyoona miradi ya maendeleo inavyozidi kuzinduliwa.

Diwani Manga (katikati) na wanakijiji wa Tegelea wakiwa katika shangwe na nderemo katika uzinduzi huo.

Ahmed aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha katika miradi ya maendeleo kama hiyo.

Kwa upande wake mwanzilishi wa ujenzi wa kituo hicho, Dokta Yasir ambaye ni bingwa wa tiba za watoto alikipongeza Chama cha Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya chama hicho na kusaidia kuikamirisha zahanati hiyo na kupunguza au kuondoa hadha waliyokuwa wakikumbana nayo kijijini hapo kwenda umbali mrefu kusaka matibabu haswa kinamama waliokuwa wakitaka kujifungua.  HABARI/PICHA NA ISSA MNALLY WA GLOBAL PUBLISHERS 

Leave A Reply