The House of Favourite Newspapers

DJ Khaled ‘Life Style’ Yake ni Balaa

DJ Khaled

U NAMFAHAMU, unampenda na pengine huwezi kujitenga naye. Hivyo ndivyo ambavyo DJ Khaled ameingia kwenye maisha yako, akilini mwako na pengine umejikuta unamsikiliza kila mara kabla ya kulala, asubuhi ukiamka au ukiwa kwenye mishemishe zako.

 

Kiukweli ni vigumu kukumbuka ni lini jamaa huyu ambaye jina lake halisi ni Khaled Mohamed Khaled hakuwa mtu maarufu, na ni sahihi kusema kutokana na mafanikio yake, jamaa kajitengenezea ‘ka-empire’ kwa ajili yake na familia yake kwenye gemu la muziki duniani.

 

 

 

 

Unaweza kujiuliza kutokana na mafanikio yake, jamaa ana utajiri wa kiasi gani siyo? Sawa, endelea kusoma kwa kina!

 

Kwanza, kumuita Khaled, DJ pekee haitoshi. Ndiyo, ni msugua santuri lakini mbali na hilo ni muandaaji wa muziki, anamiliki lebo, ni mtangazaji na mwandishi.

Zaidi yupo vizuri katika kulifagilia jina lake kwenye nyimbo mbalimbali, kwa mfano utamsikia akipiga kelele kwa kusema (Listen carefully, I bet you can hear it in your brain right now.)

 

Ni rais pia wa Studio ya Def Jam South na muanzilishi wa Kampuni ya We the Best Music Group. Kwani hujawahi kumsikia kwenye nyimbo mbalimbali akisema, “We the Best”?

Hata hivyo hizo bado si habari za kukufurahisha kuhusu DJ Khaled, zaidi ya hizo jamaa anamiliki kampuni nyingine iitwayo All I do Is Win, ana hisa kwenye brand ya kinywaji cha Belaire Rose na anaingiza zaidi ya bilioni 20 za Kibongo kupitia madili kutoka kwenye makampuni ya Mentos, Champ Sports na Apple.

 

Lakini akiwa hata haingii kwenye 10 bora ya ma-DJ wenye mkwanja mrefu duniani, ni maarufu zaidi na utajiri wake kutokana na dili zote anazofanya ni dola milioni 20 ambazo ni zaidi ya bilioni 45 za Kibongo.

 

 

NYUMBA ANAYOLALA

Jamaa anaishi kwenye mjengo wa maana ambao unaweza kuuita hekalu, ngome, himaya au majina utakayoamua ya kukuchekesha ambao upo kwenye Kilima cha Beverly, ambao umemgharimu dola za Kimarekani milioni 10, zaidi ya bilioni 20 za Kibongo.

Ndani ya mjengo huo, kuna swimming pool, miti ya mianzi iliyopangiliwa vizuri, maua ya kuvutia na mimea mbalimbali.

Mbali na mjengo huo, DJ Khaled anamiliki mjengo mwingine huko Miami, Florida uliomgharimu dola milioni 4, zaidi ya bilioni 8 za Kibongo.

MAGARI ANAYOENDESHA

Jamaa anaendesha magari makali ya bei mbaya ambayo ni pamoja na Rolls Royce Wraith Coupe, Ghost Sedan, Phantom VIII, Cadillac Escalade na Range Rover.

SAA ANAZOVAA

Jamaa anajipenda balaa. Mbali na raba za maana anazovaa mguuni kutoka brand kubwa duniani, cheni za dhahabu, saa anazovaa si za kitoto. DJ Khaled anapendelea saa za Fancy, Rolex na Hublot.

 

KAWEKEZA KWA MWANAYE

Mwanaye wa kiume, Asahd Khaled ndiye mtoto anayeishi kitajiri zaidi duniani kwa sasa. Akiwa na mwaka mmoja na miezi tisa tu mtoto huyu anayetupia viwaro vya suti za Gucci, viatu vya Jordan na saa iliyogharimu zaidi ya milioni 200 za Kibongo, ameanza kuingiza mkwanja mrefu kutokana na baba yake kuwekeza pesa kwake kumbrandi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Alpha Life, unasema kwamba DJ Khaled kawekeza kwa mwanaye huyo robo ya fedha zake ili kuhakikisha anaishi maisha ya kistaa!

Comments are closed.