The House of Favourite Newspapers

Djuma: Narudi Tena Simba

Masoud Djuma

BAADA ya kumalizana vizuri na mabosi wake wa zamani wa Simba na kubeba kilichokuwa chake, aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Mrundi, Masoud Djuma, amesema anaondoka lakini ipo siku atarudi tena Msimbazi.

 

Championi Jumatano linajua Simba na Djuma wamefikia makubaliano mazuri ya kumlipa shilingi milioni 17 kama kifuta jasho na kigogo mmoja amem­pa fedha ya mafuta ya gari yake.

 

Djuma amefikia makubaliano hayo ya kuachana na Simba baada ya uongozi chini ya mw­wekezaji wao, Mohammed Dewji kushindwa kusuluhisha ugomvi uliokuwepo kati yake na bosi wake Mbelgiji, Patrick Aussems.

 

Mrundi huyo leo Jumatano anaondoka nchini kurejea Rwanda kwa gari lake ambalo alikuja nalo alilokuwa analitumia hapa nchini katika mizunguko yake.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Djuma ambaye huenda akaibukia African Lyon kama Kocha Mkuu, alisema hajaondoka Simba kwa ubaya na anafurahia sapoti kubwa aliyokuwa anaipata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo ambayo anaamini ndiyo itakayomrejesha tena kwenye timu hiyo.

 

“Kila jambo ujue lina wakati wake na hili lililonikuta ndiyo limefikia wakati wake, hivyo acha niondoke zangu na kikubwa ninaiombea Simba ifan­ye vizuri katika kila mashindano itakayoshiriki.

 

“Simba hapa ni nyumbani ninaamini ipo siku nitarejea tena kuifundisha, Mungu ak­ipenda kwani sikutarajia kama ipo siku ningekuja kuifundisha timu kubwa kama hii.

“Nashukuru nilifanya kazi yangu vizuri sana Simba, lakini ndiyo hivyo hali hiyo iliyotokea ndiyo ikanisababishia mimi niondoke zangu Simba,”alisema Djuma ambaye mashabiki wa Simba walimkubali.

Stori na Wilbert Molandi, Championi Jumatano

 

Comments are closed.