Djuma: Simba Wagumu Ila Tutawachapa

BEKI mpya kisiki wa Yanga, Mkongomani Djuma Shaban, amefunguka na kueleza kuwa mechi yao na Simba itakuwa ngumu lakini wamejipanga kushinda mechi hiyo.

 

Kwa mara ya kwanza Djuma ataitumikia Yanga kwenye mechi hiyo ya dabi wakisaka taji la Ngao ya Jamii itakayopigwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Djuma amesema kuwa: “Najua utakuwa ni mchezo mgumu sana kwetu ila tumejipanga na tupo makini sana kuweza kushinda mchezo huo kwani ni muhimu sana kwetu. Itakuwa dabi yangu ya kwanza na nina imani itakuwa nzuri kwa upande wetu.”

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam


Toa comment