Dk 270 Ajibu Apangua Mfumo wa Aussems Simba

Ibrahim Ajibu.

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji amekoshwa na uwezo ambao ameuonyesha kiungo mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu katika michezo mitatu ya kirafi ki ambayo amecheza huku akienda mbali kuwa anafi kiria kubadilisha baadhi ya mbinu zake kwa ajili ya kiungo huyo.

 

Aussems amemtumia Ajibu katika michezo mitatu ya kirafi ki ambayo ni sawa na dakika 270 ambayo Simba wamecheza hivi karibuni wakati Ligi Kuu Bara iliposimama kupisha kalenda ya michezo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Kiungo huyo alianza kwenye mechi dhidi ya Bandari FC iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar na mechi mbili dhidi ya Mashujaa FC na Black Eagle ya Burundi ambapo alifunga bao moja dhidi ya Bandari.

 

Kocha huyo ameliambia Championi Ijumaa, kuwa kiungo huyo ameonyesha uwezo wa juu katika mechi hizo huku akifi kiria juu ya kupangua mbinu zake kwa ajili ya kiungo huyo kucheza.

“Kwenye mechi hizi tatu nimemtumia katika maeneo tofauti ikiwemo mshambuliaji kamili kwenye mechi na Bandari FC ambapo nililazimika kufanya hivyo kwa sababu Wilker aliyecheza naye alikuwa amechoka na nilikuwa na wachezaji vijana kwenye benchi.

 

“Lakini kitu kikubwa ni kuwa ameonyesha uwezo na nafi kiria wapi nimchezeshe baada ya mechi hizi kupita, lakini pia wachezaji wengine nao wameonyesha viwango vyao na niwapongeze kwa hilo,” alisema Aussems.

SAID ALLY, Dar es Salaam

MWAKINYO: “Watanzania Wajekushuhudia ARNEY TINAMPAY Akipigwa”


Loading...

Toa comment