The House of Favourite Newspapers

DK BASHIRU: Nimemwagiza Lugola Anipe Maelezo, Haiwezekani! – Video

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Bashiru Ally, amesema amempa maagizo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ampe maelezo kwa nini polisi wanawanyanyasa waendesha bodaboda, ikiwa ni pamoja na kuwalipisha ushuru tofauti naulioandikwa kwenye leseni, na kwa nini wanawakamata hata kama hawana makosa.

 

Dkt. Bashiru ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na mambo mengine, amempokea aliyekuwa Mbunge wa Liwale kwa tiketi ya CUF, Zuberi Kuchauka aliyerejea CCM.

VIDEO: MSIKIE HAPA BASHIRU AKIZUNGUMZA

Comments are closed.