The House of Favourite Newspapers

Dk. Bilal, Pinda waongoza mamia katika maziko ya Waziri Kombani Moro

0

KOMBANI MAZIKO MORO (5)

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Kombani.

kombani maziko (1)

Spika wa Bunge, Anne Makinda akiweka udongo katika kaburi la marehemu Celina Kombani. Nyuma yake ni Samia Suluhu.

KOMBANI MAZIKO MORO (6)

Mama Salma Kikwete naye akiweka udongo kwenye kaburi la Kombani.

kombani maziko (2) kombani maziko (3)

Bwana Hemed Saleh Pongoleni ambaye ni mume wa marehemu akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake, Celina Kombani.

kombani maziko (4) kombani maziko (5)

Watoto wa marehemu wakiwa na mashada ya maua wakati wa maziko ya mama yao.

KOMBANI MAZIKO MORO (11)

Viongozi mbalimbali wakishiriki maziko hayo.

KOMBANI MAZIKO MORO (2)-001

Jeneza lenye mwili wa marehemu Celina Kombani likiingizwa kaburini.

KOMBANI MAZIKO MORO (12)

Jeneza likiombewa kabla ya kuingizwa kaburini.
KOMBANI KUAGWA (1)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho mbele ya mwili wa Waziri Celina Kombani katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.

KOMBANI KUAGWA (2)

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akiaga mwili wa Waziri Kombani leo.

KOMBANI KUAGWA (3)

Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake mbele ya jeneza lenye mwili wa Waziri Celina Kombani kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

KOMBANI KUAGWA (4)

IGP Mstaafu, Omar Mahita naye akitoa heshima zake za mwisho.

KOMBANI KUAGWA (7)

Baadhi ya wasanii wakitoa heshima zao za mwisho.

MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda leo wameongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani yaliyofanyika kwenye shamba lake lililopo Lukombe nje kidogo ya Mji wa Morogoro.

Kombani ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki alifariki dunia Alhamisi iliyopita katika Hospitali ya Andhraprasth Appollo ya mjini Delhi, India alikokuwa amelazwa akitibiwa saratani ya kongosho.

Viongozi wengine walioshiriki maziko ya Mhe. Kombani ni pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Spika wa Bunge Anne Makinda, Mgombea Mwenza wa urais kupitia CCM Samia Suluhu, IGP Mstaafu Omar Mahita na wengineo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Celina Kombani mahali pema peponi. AMEN.

(PICHA ZOTE NA DUNSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)

Leave A Reply