The House of Favourite Newspapers

Dk. Fadhili awapa somo la uzazi mastaa

0

DOKTA-FADHILI-AMZAWADIA-ZARI-BAISKELIIMELDA MTEMA,

Daktari wa Kitengo cha Sayansi na Tiba Asili kilichopo Mbezi-Afrikana, Fadhili Emilly ambaye ni mdhamini wa fursa ya wasomaji kujipatia Tv Flat Screen inayotoka kwenye gazeti hili, ameibuka na somo la uzazi kwa mastaa wa Bongo.

Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzi, Dk. Fadhili alisema wapo mastaa wanahangaika kupata watoto, hivyo yeye anawapa somo ili wajue njia gani mjamzito anatakiwa kutumia ili ampate mtoto anayemtaka.

“Unaweza kupata  mtoto anayefanana na mama yako au nduguyo yeyote. Lakini pia wajue kuna uwezekano wa kupata mtoto anayefanana na baba mwenye nyumba wakati hajalala naye.

“Au mtoto anazaliwa anafanana na watoto wa mpangaji mwanaume. Watu wanashikana uchawi. Kuna sababu hata kama mjamzito atakuwa hajalala na huyo mpangaji.

“Mjamzito akimchukia mtu kutoka moyoni, lazima atazaa mtoto wa kufanana naye. Ndiyo maana wapo wanaozaa watoto wamefanana na majirani zao.

“Lakini kuna ishu hii ya kuzaa mapacha. Wengi wanadhani hufuata ukoo. Si kweli. Mwanamke yeyote anaweza kuzaa mapacha. Mwanamke akishakutana kimwili na mwenzake akiwa katika siku za hatari, anatakiwa awe na tabia ya kujigeuzageuza kitandani. Uwezekano wa kuzaa mapacha ni mkubwa.

“Kuna hata mapozi anayotakiwa kuyatumia mwanamke mwenye matatizo ya kupata ujauzito ambapo ni lazima ayatumie ili apate,” alisema dokta huyo.

Leave A Reply