The House of Favourite Newspapers

Dk Fadhili: Wolper ni ‘Wife Material’

0
Dk Fadhili Emily .

TABIBU maarufu Bongo, Dk Fadhili Emily ameibuka na kumkingia kifua muigizaji Jacqueline Wolper kuwa anafaa kuwa mke wa mtu tofauti na tuhuma zinazoenezwa mitandaoni kuwa mrembo huyo hajatulia.

Dk Fadhili ambaye aliwahi kutajwa kubanjuka na mrembo huyo kisha kumwagana, alisema kwa sababu tu yeye sasa ameokoka kwa sasa na amepata mtu mwingine lakini vinginevyo, angeweza kumuoa Wolper.

Wolper.

“Nimeona kwenye mitandao, wanamuandama kuwa hajatulia na kwamba ana msururu mkubwa wa wanaume ambao ametembea nao, kimsingi huyu mrembo hajapata tu mtu sahihi lakini anafaa kuwa mke wa kulea familia kabisa,” alisema Dk Fadhili ambaye kliniki yake iliyopo maeneo ya Mbezi- Afrikana, Dar ilikumbwa na panga la wizara ya afya lililofungia kliniki hizo kwa kutokidhi masharti ya serikali.

 

NA MWANDISHI WETU | IJUMAA WIKIENDA | OVER ZE WEEKEND

 

Sikia Kauli ya Lulu kwa Ally Remtullah Mbunifu wa Mavazi

Leave A Reply