Mgombea urais wa CCM, Dk. Magufuli akishuka kwenye gari kwenda kuhani msiba wa mwalimu wake, Cornel Pastory.
Dk. Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la mwalimu wake huko wilayani Biharamulo.
Dk. Magufuli akisali katika kaburi la mwalimu wake.
Dk. Magufuli akimfariji mke wa marehemu, Bi. Paskazia Mofuruku.
Kaburi la mwalimu Cornel Pastory.
Mwalimu Cornel Pastory enzi za uhai wake.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli leo alikwenda Kijiji cha Nyakatuntu kilichopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera kuhani msiba wa mwalimu wake aliyemfundisha Shule ya Msingi Chato.
Mwalimu huyo aitwaye Cornel Pastory alimfundisha Magufuli tangu darasa la kwanza na alifariki dunia Agosti 7, 2015.
Akiwa msibani hapo, Magufuli aliwapa pole wafiwa na kumfariji kwa dakika kadhaa mke wa marehemu, Bi. Paskazia Mofuruku.
(Picha zote na Richard Bukos / GPL, Biharamulo)