The House of Favourite Newspapers

Dk Shika Atamba Kutikisha Usiku wa 900 Itapendezaa (Video)

0
Meneja wa Dk. Shika, Catherine Kahabi (katikati) akizungumza na wanahabari, kulia ni Dk Shika.

YULE daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu aliyejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini siku za hivi karibuni kufuatia kufika dau wakati wa mnada majumba bilionea Lugumi yaliyopo jijini Dar es Salaam, Dkt. Louis Shika ametamba kuwa atafanya kweli katika event ya Usiku wa 900 Itapendeza.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 30, 2017, Dk Shika alisema; “Ninatarajia usiku wa 900 Itapendeza nitaongea na wakazi wa Dar es Salaam, tutazungumza mengi, nawaomba wajitokeze, nimejiandaa vyema, karibuni nyote tuzungumze, itapendeza mkifika nyote,” alisema Dkt. Shika.

Dk Shika akizungumza na wanahabari.

Aidha katika hafla hiyo itakayofanyika Desemba 9, 2017 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem jijini Dar, burudani kibao zitapigwa zikiwemo kutoka kwenye bendi za Twanga Pepeta, Jahazi Modern Taarabu, wasanii wa Bongo Fleva na mchekeshaji maarufu nchini, Mc Pilipili.

Dk Shika anatarajiwa kufunguka mengi ikiwemo maisha yake aliyoyapitia, masomo ya udaktari, maisha yake nchini Urusi hadi aliporudi Tanzania pamoja na kutoa hamasa kwa vijana hususani katika mambo ya ujasiliamali.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

VIDEO: MSIKIE DK SHIKA AKIFUNGUKA

Leave A Reply