The House of Favourite Newspapers

DK TULIA: NIKIKUTANA NA JPM NITAMWAMBIA HAYA KUHUSU GLOBAL GROUP

Dk Tulia Ackson akikaribishwa katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, leo na Mhariri Mtendaji, Saleh Ally.

DAR ES SALAAM: Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson Mwansasu, Jumamosi Februari 23, 2019  alitembelea ofisi za Kampuni ya Global Group na kueleza namna alivyoguswa na utendaji kazi wake unaozingatia weledi wa utoaji wa habari.

Dk Tuli akisaini katika kitabu cha wageni.

Global Group yenye makao yake makuu Sinza-Mori jijini Dar ni wachapishaji wa magazeti yanayosomwa zaidi nchini Tanzania ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, Championi na Spoti Xtra. Pia ni wamiliki wa runinga na redio za mtandaoni za Global TV Online na +255 Global Radio.

Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho akimkabidhi Dk Tulia, tuzo ya Gold Play Button ambayo YouTube iliitunuku Channel ya Global TV Online baada ya kufikisha subscribers milioni moja (1,000,000) mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na wafanyakazi wa Global Group, Dk Tulia aliipongeza kampuni hiyo kwa kazi kubwa ya kuwahabarisha wananchi ndani na nje ya nchi huku akiahidi kwamba akikutana na Rais Dk John Pombe Magufuli (JPM) atamweleza mambo makubwa aliyokutana nayo ndani ya kampuni hiyo.

Dk Tulia akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Global Group kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisini hizo.

Mbali na pongezi, Dk Tulia alisema atamweleza kuwa Global Group wanafanya kazi kubwa ya kuhabarisha watu, lakini kubwa zaidi ni kuzingatia weledi.

Dk Tulia Ackson akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph.

Kwenye eneo hilo la weledi, Dk Tulia aliwataka waandishi wa Global kutokubali kutumika kupeleka jambo la upotoshaji kwa wananchi kwani kwenye siasa kuna mambo ambayo huzungumzwa kisiasa tu bila kujali ukweli wake.

Dk Tulia ndani ya studio za Global TV.

Pia alisema Global Group ni kampuni iliyojipanga kwa uhakika kuwahudumia wananchi kutokana na vifaa vya kisasa alivyovishuhudia.

Mhariri wa Gazeti la Amani, Eric Evarist akimwonesha Dk Tulia gazeti hilo.

“Unapokuwa nje ya Global huwezi kujua yaliyomo ndani, lakini nimeshuhudia mambo makubwa mno.

 

“Kwa kweli hongereni kwa kazi kubwa mnayoifanya. Nimeona vifaa vya kisasa, nimekubali mmejipanga vilivyo. Lakini kikubwa zaidi ni namna mnavyotumia weledi wenu kwenye habari, muendelee hivyohivyo kuzingatia weledi,” alisema Dk Tulia.

Dk Tulia akisalimiana na mwandishi wa Championi, Sweetbert Lukonge.

 

Kiongozi huyo alisema alishuhudia namna ambavyo kampuni hiyo ilivyotoa ajira nyingi kwa vijana.

“Nikikutana na Rais Dk John Pombe Magufuli hayo ndiyo mambo ambayo nitamweleza kuhusu Global Group. Lakini kubwa zaidi ni namna ambavyo Global Group imetoa ajira kwa vijana wengi.

Dk Tulia akizungumza na wafanyakazi wa Global.

“Siyo kwa Magufuli tu, lakini pia nikikutana na mtu yeyote nitawaeleza hayo ambayo nimeyashuhudia na niwapongeze tena kwa kazi kubwa mnayoifanya,” alisema Dk Tulia.

Mbali na kuzungumzia aliyoyashuhudia Global, Dk Tulia alizungumzia namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojikita katika kufanya kazi kwa kutaka matokeo.

Alisema Serikali chini ya Rais Magufuli ni Serikali sikivu ambayo inafanya kazi nzuri mno kwa wananchi wake.

Dk Tulia akisalimia na Mkuu wa Idara ya Digitali na IT, Edwin Lindege.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano haitaki mazoea na ni Serikali ya tofauti inayotaka kuona matokeo na mambo yakifanyika.

Dk Tulia akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Samson Mfalila.

“Rais Magufuli hataki mambo ya makaratasi, hataki mambo ya vikao na kuwa kwenye mchakato, anataka kuona vitu vinafanyika ndiyo maana unamuona kwenye hafla mbalimbali za kupokea ndege mpya au kuona mataruma kumi yameongezeka na kuwa 11,” alisema mwanamama huyo ambaye ni mbunge wa kuteuliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk Tulia katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global Group.

Comments are closed.